Wednesday, January 23, 2013

Tangazo kwa wanafunzi wote wa BAPRM TWO-SAUT MWANZA

Jamani nimepewa vitabu na mwalimu Jota wa Enterpreneur ninavyo ktk flash amesema kila mtu asome,mara nyingi nipo chuo na nitavipeleka kwa dada Irene - Stationery tafadhali sana anayetaka anitafute 0712 553 980
by Dova Mcheshi- Mbunge PR TWO A

Monday, January 21, 2013

JE,HUU NI UBINADAMU???


Na;Dovakmwene John Mscheshi


Kifo ni kitu kinachoweza kumtokea mtu yoyote na wakati wowote kwani tunaamini ni mipango ya Mungu. Kifo hutokea katika mazingira tofauti ikiwa ni pamoja na maradhi, ajali mbalimbali, vita/mapigano, ugomvi na kadhalika.
Vifo vipo vya ghafla pasipo kutarajia, vingine vikitokana na kuugua muda mfupi au mrefu. Mtu anapofariki shughuli za mazishi huandaliwa ambapo waombolezaji hukusanyika nyumbani kwa marehemu au sehemu iliyopangwa na wanafamilia kwa msiba.
Pale kwenye maombolezo huwa na pilikapilika nyingi huku ratiba ya maandalizi ikitangazwa kila inapobidi. Waombolezaji huonekana katika makundi wakiteta huku wengine wakiwa wamejawa na simanzi.
Pamoja na ukweli huo, tabia hizi hazipendezi. Kwa mfano, lipo jambo moja au niseme tabia ambayo imezoeleka kwa waombolezaji wengi kuonekana wakijadili zaidi chanzo cha kifo cha marehemu badala ya kutafakari hatma yao waliobaki duniani na kumuombea aliyetangulia mbele za haki.
Kwa maneno mengine, wapo watu wanaogeuza msiba kama vijiwe vya kumjadili marehemu. Na watu hawa, hata wakati wa uhai wake hawakuwa kusema juu yake hadharani penye kadamnasi ya watu, lakini leo kafariki wanazusha hata yale yaliyofichika. Hebu tujiulize, hivi yanahusu? Na kwanini wanadamu tuko hivi? Hii ni kasoro kubwa sana yafaa tubadilike.
Utasikia fulani wakati wa uhai wake alikuwa anaringa sana. Ebo! Ulitaka afanyeje. Hivi hujui maringo ni afya na kinyume chake ni kasoro? Kuringa ni kujisikia furaha kwa uhai wako. Ndio, usibishe.
Mara utasikia fulani alikuwa kiruka njia, alipenda sana wanaume au wanawake, alipenda sana wake au waume za watu…Oh, ameacha watoto wa baba tofauti, amekufa na gonjwa baya, eti angezingatia ushauri wa daktari yasingemsibu hayo, ili mradi ni maneno ya hovyo, kisa anayezungumzwa ameshajifumzikia.
Wengine utasikia eti laana ya baba au mama yake ndio imemuua. Ili mradi mtu atoe neno kinywani mwake kufurahisha jopo pale kwenye maombolezo. Hili siyo jambo zuri hata kidogo, hasa ikizingatiwa kuwa kila mtu anayo mapungufu yake na hakuna atakayeishi milele nikiamini kile alichowahi kuniambia bibi yangu kuwa “Uyana nyi maseiyano” yaani “Dunia ni mapishano”.
Tabia nyingine inayokera wakati wa msiba ambayo wengi bado wanaiendekeza ni kule baadhi ya ndugu kugombea mali za marehemu zikiwemo nguo zake. Eti kufa kufaana na kwamba aliyekufa kafa hivyo mali zake ni halali kwa wengine. Lo! Makubwa kwani madogo yana unafuu.
Nimewahi kushuhudia ndugu wakichukua nguo za marehemu kwa kuzificha na kuondoka nazo, tena mwili wa marehemu ukiwa bado chumba cha maiti hospitalini. Yaani mwili haujazikwa, tayari watu wanajigawia mali zake. Ni tabia mbaya sana hii. Wenye tabia hii wasidhani ni kirahisi hivyo, yapo madhara yake. Kwanini mtu asisubiri kupewa mali chini ya taratibu za kifamilia?
Lingine ambalo halina sura nzuri walifanyalo wanadamu ni kule kukimbilia kuuona mwili wa marehemu wakati hapa alipokuwa mgonjwa hakuwahi kwenda kumjulia hali achilia mbali kumsaidia fedha za matibabu. Hukimbilia kuona kafa na afya yake au kakonda? Acheni jamani, mzaha huu, ni dhambi.
Mpenzi msomaji, hebu niulize; lipi ni jema katika haya mawili:- kumtembelea mgonjwa na ikibidi kumsaidia fedha za matibabu au kule kwenda mchanga rambirambi baada ya kufa?
Wapo wale ambao hawakujua fulani alikuwa mgonjwa, lakini wakasikia amefariki. Lakini wengine, pengine mahasimu waliowahi kukwaruzana, wakisia fulani kafa huachia; “acha afe”. Yaani hawaoni kwamba hiyo ni njia yao pia. Huu siyo ubinadamu. Maisha ya mtu yanapotoweka lazima usikitike kwani hutamuona tena katika maisha haya ya kidunia. Na utambue nawe kifo kinakusubiri.
Nakumbuka bibi mzaa mamangu wakati wa uhai wake kila nilipomtembelea alikuwa anafurahi sana pale ninapompelekea zawadi ambapo husema; “Afadhali uniletee watati ningali hai, kwani nikishafumba macho(kufa) utakachoniletea ni bure”. Yalikuwa ni maneno yaliyobeba ujumbe mzito sana.
Ndio maana ni muhimu sana hata pale mwenzako anapokuwa mgonjwa yafaa tumhudumie kwa nguvu zote, tumsaidie chakula, dawa badala ya kusubiri azimike ndipo tupige mikono mifukoni kutoa rambirambi.
Sisemi watu wasitoe rambirambi, la hasha. Ninachosema hapa ni kwamba tutizame mazingira yenyewe, kama ni kifo cha ghafla ni sawa. Lakini kama ni kifo kinachotokana na maradhi tusaidiane wakati wa uhai badala ya kubezana. Pengine msaada wako unaweza kumsogezea mgonjwa maisha akakamilisha mipango yake duniani au hata akapona kabisa. Maisha Ndivyo Yalivyo.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI     

Ajali yaua mmoja MBEYA.




Mtu mmoja amekufa papohapo na wengine 48 kujeruhiwa vibaya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Jijini Mbeya kwenda Dar es Salaam kupinduka kwenye mteremko mkali wa Mlima Inyara nje kidogo ya Jiji la Mbeya.

Ajali hiyo mbaya ilitokea jana majira ya saa 1:30 asubuhi ikihusisha basi la kampuni ya Nganga Express lenye namba za usajili T 413 AVU lililoondoka Mbeya majira ya saa 1:00 kuelekea Dar es Salaam.

Akisimulia jinsi ajali hiyo ilivyotokea, dereva wa basi hilo, Alex Bunyinyiga alisema alipofika kwenye mteremko wa mlima Inyara, mahali ambapo pia kuna kona kali, aliona lori kubwa lililokuwa limeegeshwa upande wa kulia wa barabara.

Alisema alipolikaribia lori hilo, ghafla lilitokea gari lingine aina ya Fuso ambalo lilipita lori lililoegeshwa na kumfuata upande wake, hali ambayo ilisababisha watake kugongana uso kwa uso.

“Baada ya kuona tunaenda kugongana uso kwa uso, niliamua kukwepesha gari langu upande wa lori lililokuwa limeeegeshwa upande wa kulia kwangu na nikafanikiwa kulipita lori hilo kwa upande wake wa kulia, lakini nilipojaribu kurudisha gari langu likae barabarani liligoma na ndipo likapinduka,” alisema Bunyinyiga.

Shuhuda mwingine wa ajali hiyo, Noa Elias alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori aina ya fuso ambaye aliamua kulipita lori lililoharibika barabarani bila tahadhari na kutaka kugongana uso kwa uso na basi la Nganga.

Muuguzi wa Zamu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, Bilhuda Feruz amethibitisha kupokea majeruhi 48 na wanane kati yao wamelazwa na hali zao zinaendelea vizuri.

Hata hivyo, takwimu hizo zimetofautiana na zile zilizotolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman ambaye alidai kuwa majeruhi walikuwa ni 53 nwa kwamba 45 kati yao walitibiwa katika Hospitali ya Rufaa na kuruhusiwa huku majeruhi wanane wakilazwa hospitalini hapo kwa matibabu zaidi.

Kamanda Diwani alimtaja mtu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Enock Lwila mkazi wa Mama John Jijini Mbeya.

Alisema marehemu huyo alikuwa na Sh. milioni 13 mfukoni ambazo ziliokolewa na askari waliowahi kwenye eneo la tukio.

Kamanda Diwani alisema kuwa kwa sasa fedha hizo ziko salama mikononi mwa Polisi na kuwa baada ya kupatikana kwa ndugu halali wa marehemu atakabidhiwa.

 
CHANZO: NIPASHE     

RC Lindi alazwa,Pinda amtembelea


Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila, amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

Akizungumza na NIPASHE jana mmoja wa wanafamilia ambaye alipokea simu ya Mkuu huyo wa mkoa alisema Mwananzila amelazwa hospitalini hapo tangu Jumatano ya wiki iliyopita.
Alisema Waziri Mkuu Mizengo Pinda amemtembela jana kumjulia hali na kwamba hata hivyo anaendelea vizuri na madaktari wamekuwa karibu naye kumtibu.

Naye Ofisa habari wa Muhimbili, Aminael Aligaesha, alisema Mkuu wa Mkoa wa Lindi hali yake inaendelea vizuri ukilinganisha na siku alipopelekwa hospitalini hapo.

OKAH matatani huko Afrika kusini








Mahakama nchini Afrika Kusini imempata na hatia ya vitendo vya kigaidi kiongozi wa waasi wa Nigeria Henry Okah.

Okah anasemekana kupanga mashambulizi ya mabomu yaliyotegwa ndani ya gari na kuwaua watu 12.
Taarifa zinazohusiana
Afrika

Okah alipatikana na hatia ya makosa 13 kuhusiana na vitendo vya kigaidi.

Alikamatwa mjini Johannesburg siku moja baada ya mabomu mawili kulipuka wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Nigeria.

Alikanusha makosa hayo ingawa kundi analoongoza la Mend, lilikiri kutekeleza mashambulizi hayo.

Jaji wa mahakama kuu mjini Johannesburg, Neels Claassen, alimpata na hatia Okah ya makosa ya kupanga njama ya mashambulizi pamoja na kufanya vitendo vya kigaidi ikiwemo kulipua mabomu.

"ushahidi ambao ulitolewa na washirika wake haukupingana,'' alisema jaji Claassen

Okah alikamatwa kwa kosa la kumiliki bunduki kinyume na sheria nchini Angola mwaka 2007 na kisha kuhamishwa hadi nchini Nigeria ingawa hakuwahi kuhukumiwa.

Aliachiliwa baada ya miaka miwili chini ya msamaha uliotolewa kwa wapiganaji walio katika maeneo ya mafuta na ndipo aliporejea Afrika Kusini ambako aliishi hadi mwaka 2003.

MAN UNITED YABANWA.


Robin Van Persie aliiwezesha timu yake ya Manchester United kuongoza kipindi cha kwanza baada ya kufunga bao katika dakika ya 25.
Taarifa zinazohusiana
Kandanda, Uingereza

Van Persie alipata goli hilo akiunganisha krosi ya Tom Cleverly.

Man United wakiamini kuwa tayari wamepata ushindi katika mechi hiyo, walijikuta wakigawa pointi baada ya Clint Dempsey kufunga katika dakika za majeruhi na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa Tottenham katika uwanja wao wa White Hart Lane.

Matokeo hayo bado yanaiacha Manchester United kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na pointi 56, huku ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 51.

Tottenham iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 41, pointi nne nyuma ya Chelsea yenye pointi 45, ikikakalia nafasi ya tatu ya ligi kuu ya England.

Timu zote hizo nne zimecheza mechi 23 kila moja.




MALI YAVUNA POINTI 3 MUHIMU-AFCON




Seydou Keita Keita baada ya kufunga bao lake la kwanza dhidi ya Niger


Mali inayopewa nafasi ya kusonga katika hatua ya makundi, ya michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika, mwaka huu, imeandikisha ushindi wake wa kwanza katika mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Niger.

Mali iliilaza Niger bao moja kwa bila katika mechi hiyo ya pili ya kundi B.

Seydou Keita, nahodha wa timu ya Mali, alifunga bao hilo la ushindi katika dakika ya 84 baada ya mlinda mlango wa Niger, Daouda Kassaly, kuutema mpira wa adhabu na kumfikia mfungaji.

Kwa matokeo hayo Mali, sasa inaongoza kundi B ikiwa na pointi tatu na goli moja.

Timu za DRC na Ghana zinafuatia katika msimamo wa kundi B, zikiwa na pointi moja kila moja baada ya timu hizo mbili kutoshana nguvu ya kufunga magoli mawili kwa mawili.

Hapo kesho mechi za kundi C, zinaanza huku mabingwa watetezi Zambia wakimenyana na Ethiopia, nayo Nigeria ikivaana na Burkina Faso.

Thursday, January 10, 2013

GANG MAN STYLE YAMPIKU JUSTIN BIEBER




MATOKEO YA LEO HISPANIA

Spanish Copa del Rey
Final - Getafe 0-0 Atletico Madrid

Final - Barcelona 5-0 Cordoba
*Thiago(17')
*David Villa(21')
*David Villa(26')
*Alexis Sánchez(55')
*Alexis Sánchez(85')

Final - Real Betis 1-0 Las Palmas
*Rubén(85')

JE! Una mkumbuka huyu?


VICKY KAMATA.,UBUNGE+MUZIKI

Mh.Vicky Kamata
Nyota muziki, siasa aliyejitosa kusaidia walemavu
“Huwa najisikia vibaya kuona walemavu na watu wasiojiweza wakitaabika kwa kukosa mahitaji yao muhimu. Ndiyo maana nikashawishika kuanzisha taasisi ya Victoria Foundation kwa nia ya kuhakikisha kwamba nami nasaidia kadri ya uwezo wangu harakati za kuwainua walemavu na wasiojiweza,” ndivyo anavyoanza kusema Mheshimiwa Vicky Kamata, Mbunge wa Viti Maalum kutoka mkoani Geita (CCM) na msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya.

Kesi ya Papaa Msofe Yapigwa kalenda tena.

 


 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam jana imepiga kalenda
kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara maarufu jijini, Marijani Abdubakari (50), ‘Papa Msofe’ hadi Januari 22, mwaka huu itakapokuja kutajwa tena.

Hakimu Mkazi Agnes Mchome, alihairisha kesi hiyo baada ya Wakili wa Serikali Ofmedy Mtenga, kuiambia mahakama kuwa upelelezi upande wa Jamhuri haujakamilika.

TUME YA KATIBA YATOA TAMKO KALI KWA WAANDISHI WA HABARI

Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetamka rasmi kuwazuia waandishi wa habari kuhudhuria mikutano yake na makundi maalum, vikiwamo vyama vya siasa, inayoendelea kwa lengo la kukusanya maoni ya Katiba Mpya.

Kwa kauli hiyo ya Tume hiyo, sasa itategemea huruma na hisani ya makundi, ambayo yatakuwa tayari ‘kuwatafunia’ na ‘kuwalisha’ wanahabari mambo yaliyojiri, badala ya wao wenyewe kuyapata moja kwa moja na kwa uhalisia wake kutoka ndani ya mikutano hiyo.

Kauli ya kuwazuia waandishi wa habari kuhudhuria mikutano hiyo, ilitolewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba, jijini Dar es Salaam jana, kabla ya kuanza mkutano kati ya tume yake na Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD).

Jaji Warioba alitoa kauli hiyo alipoulizwa na NIPASHE kama waandishi wa habari wangeruhusiwa kuingia ukumbini kusikiliza maoni ya UMD.

Alijibu kwa kifupi kwamba waandishi wa habari hawaruhusiwi kuhudhuria siyo tu katika mkutano huo juzi, bali katika mikutano yote kati ya Tume na makundi yote.

“Hamuwezi kuingia ukumbini (kwenye mkutano) kusikiliza maoni yanayotolewa. Siyo tu tuliwazuia jana (juzi), bali hata leo (jana). Pia na siku nyingine hamtaruhusiwa kushiriki,” alisema Jaji Warioba.

Mikutano kati ya Tume na makundi hayo ilianza juzi katika ofisi za Tume hiyo na katika kumbi tofauti za jengo la Karimjee, jijini Dar es Salaam.

Katika ofisi za Tume, mikutano hiyo inaongozwa na Jaji Warioba pamoja na mjumbe wa Tume hiyo, Profesa Mwesiga Baregu.

Katika kumbi za jengo la Karimjee, baadhi ya mikutano inaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Augustino Ramadhan na maofisa wengine wa Tume hiyo.

Katika mikutano yote hiyo, baadhi ya maofisa wa Tume, wamekuwa wakiwazuia waandishi wa habari kuhudhuria.

Askari polisi wauwawa huko Ngara

 Askari wawili wa Jeshi la Polisi wa Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, wameuawa kwa kupigwa na wananchi wenye hasira na  gari lao kuchomwa moto, wakidhaniwa kuwa ni majambazi.

Tukio hilo lilitokea katika Kijiji cha Kasheshemisha, Kata ya Rugu Wilaya hiyo juzi saa 2:30 usiku.

Akitoa maelezo mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Karagwe chini ya Mkuu wa Wilaya  hiyo,  Darry Ibrahim Rwegasira na ya Mkoa iliyoongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoa huo,  Phillipo Kalangi na viongozi wengine wa serikali wilayani humo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Kasheshemisha, Sadick Mohammed, alisema walipata taarifa kutoka Kijiji cha Rugu kuwa kuna majambazi  walifika majira ya saa 12:00 jioni na wakati wakijaribu kuondoka, wanakijiji waliweka kizuizi barabarani na kuwaamuru wasimame.

Mihamed alisema watu hao hawakutii amri na kupita kwa nguvu katika eneo hilo ndipo walipoamua kupiga simu kwa mwenyekiti huyo ambaye naye alitoa taarifa  kwa wananchi wake na kuziba barabara kwa mawe.

Alisema  gari lao lilipofika Kijiji cha Kasheshemisha, lilikuta mawe barabarani na kushindwa kupita ndipo wananchi waliwaamuru  wajisalimishe, lakini walikaidi na kuanza kufyatua risari hewani huku wakitafuta njia ya kuwawezesha kutoroka.

Alisema walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili na kutokana na hasira ya kurushiwa risasi, waliwapiga hadi kuwaua kisha walipopekua ndani ya gari walikuta meno saba ya tembo.

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, hasira za wananchi zilipanda zaidi walipogundua mwenzao amejeruhiwa na risasi na kuamua kuyatoa meno hayo ya tembo saba na kulitekeleza gari  hilo lenye namba za usajili T.654 BNB.

Mohamed alisema mwanakijiji huyo, Jovinary Joseph aliyejeruhiwa na risasi kwenye kiganja, alikimbizwa Hospitali Teule ya Wilaya ya Karagwe ya Nyakahanga kwa matibabu.

Nyoso Wa SIMBA atemwa safari ya OMAN



 

  Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam, wamemtosa beki Juma Nyosso katika safari yao ya Oman iliyoanza kwa mafungu jana kutokana na kosa la kutotii masharti aliyopewa na uongozi wa klabu hiyo.

Simba iliondoka jijini Dar es Salaam jana na kikosi cha wachezaji 14 kuelekea Oman kwa ajili ya kuweka kambi ya wiki moja ya kujiandaa na Ligi ya Kuu ya Tanzania Bara na Ligi ya Klabu Bingwa Afrika.

Wachezaji wengine waliobaki kuiwakilisha Simba katika Kombe la Mapinduzi Zanzibar na walio katika kambi ya timu ya taifa (Taifa Stars) wataungana na wenzao Oman baada ya kumaliza majukumu yao.
Waliopo katika kikosi cha Stars kilichosafiri jana kwenda Ethiopia kucheza mechi ya kimataifa ya kirafiki kesho dhidi ya wenyeji ni kipa Juma Kaseja, Amir Maftaha, Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto, Shomari Kapombe na Amri Kiemba.

Waliobaki na timu yao kusubiri kumalizika kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar ni Haruni Athuman, Abdalah Seseme, Miraji Adam, Julius Mkude na Hassan Singano.

Nyosso alirudishwa kucheza katika kikosi cha vijana wa U-20 wa klabu hiyo kutokana na utovu wa nidhamu na kushuka kwa kiwango chake, jambo ambalo beki huyo wa kati hajalitimiza.

Akizungumza na NIPASHE jana, Katibu wa Simba, Evodius Mtawala alisema Nyosso ameachwa na hatarudishwa kikosini hadi pale atakapotekeleza masharti.

"Kuna baadhi ya vitu tumesimamisha kwenye mkataba wake ikiwamo mshahara," alisema Mtawala.
Alisema atakapoanza kuvitekeleza atarejea kupata mahitaji yote kama ilivyo kwa wachezaji wenzake.

Mtawala alisema msimamo wa Simba uko pale pale kwamba beki huyo, ambaye ameripotiwa kutumia muda wake nje ya kikosi kucheza mechi za mchangani, ni lazima aende akaripoti kwenye timu ya vijana na akaonya kwamba kama ataendelea kukaidi agizo ataangukia pabaya.

Alimtaka mlinzi huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Bara aache kusikiliza ushauri mbaya na badala yake atimize masharti ya ajira yake kwa manufaa yake mwenyewe.

AJALI YA BUNDA EXPRESS

Basi la Kampuni ya Bunda Express lenye namba za usajili T 782 BKZ, likiwa kwenye maji baada ya kuacha njia na kupinduka katika Kijiji cha Ngashe Wilaya ya Magu mkoani Mwanza wakati likitoka Bunda mkoani Mara kuelekea Mtukula Kagera jana. Ajali hiyo imeua watu wawili na kujeruhi wengine 22



Chelsea yapingwa MBILI BILA na Swansea



 

 Michael Laudrup amakiri kuwa ushindi wa Swansea wa magoli mawili kwa bila dhidi ya Chelsea katika raundi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la ligi, ulikuwa wa kushangaza.
Makosa yaliyofanywa na mlinda lango wa Chelsea Branislav Ivanovic ilisababisha Michu na Danny Graham kuifungia Swansea magoli hayo katika mechi iliyochezwa katika uwanja wa Stampford Birdge.
Raundi ya pili cha mechi hiyo itachezwa tarehe 23 mwezi huu katika uwanja wa nyumbani wa Swansea.
Chelsea ilithibiti mpira kwa asilimia kubwa lakini makosa hayo yaliyofanywa na Ivanovic yalisababisha matumaini ya Chelsea ya kufuzu kwa fainali za kombe hilo kudidimia.

Monday, January 7, 2013

CHADEMA YAMTIMUA MAKAMU MWENYEKITI WA BAVICHA

 Kamati ya Tendaji ya Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema (Bavicha), linadaiwa kumtimua uongozi na kisha kumvua uanachama Makamu Mwenyekiti wake Taifa, Juliana Shonza, pamoja na wanachama wengine wawili wa Baraza hilo
Mbali na Shonza, wanachama wengine wa Bavicha, ambao wamevuliwa uanachama na Kamati Tendaji ya Bavicha, wametajwa kuwa ni waliokuwa wagombea Uenyekiti wa Baraza hilo mwaka juzi, Habib Mchange na Mtela Mwampamba.

Mchange pia amewahi kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema katika Jimbo la Kibaha Mjini katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, lakini akaangushwa na Mbunge wa sasa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sylivester Koka.(ipp media).

Rock city

TEMBELEA JIJI LA MWANZA IJIONEE BISMARK ROCKS

PAPA ATOA ONYO JUU YA MACHAFUKO HUKO NCHINI SYRIA

 Pope warns Syria could become 'a field of ruins'

Pope Benedict has urged the international community to end what he called the endless slaughter in Syria before the entire country becomes a "a field of ruins."
He made the appeal in particularly strong terms during a yearly "state of the world" address to diplomats accredited to the Vatican.

Kutoka IKULU ya Marekani.

 US President Barack Obama has named Chuck Hagel to be his next defence secretary and counter-terrorism adviser John Brennan to lead the CIA, but the nominations may not go smoothly.

KUTOKA BBC SPORTS:Adebayor abadili uamuzi.

Tottenham forward Emmanuel Adebayor has reversed his decision not to represent Togo at January's Africa Cup of Nations, leaving Spurs with Jermain Defoe as their only recognised striker.
The 28-year-old initially planned to remain with his club because of a row over team security and unpaid bonuses.
But he will now go to the tournament in South Africa, which starts on 19 January, and may miss six Spurs games.

Real Fact about Relationship.

Mahusiano ni Mazuri kama yanafanyika katika;
Muda,Mahali,Umri sahihi.

The World Amazing Football Player


The Magic MESSI


Hapa Ronaldo hana Hamu


Kikosi cha Soka cha Dunia 2012/2013


BALLON D'OR 2013

GUMZO:
Lionel Messi ashinda tuzo ya MCHEZAJI BORA WA DUNIA kwa mara ya 4 mfululizo.
Awapiku Ronaldo na Iniesta.
Tunzo Zenyewe.


FIFA Women's Player of the year-ABBY WAMBACH
FIFA Ballon d'or of the year -Lionel Messi
FIFA MENS Coach of the year-Vicente Del Bosque
FIFA Women's coach of the year-Pia SUNDHAGE
FIFA Puskas award-MIROSLAV STOCH
FIFA fairplay award-UZBEKISTAN FOOTBALL FEDERATION
FIFA Presidential award-FRANZ BECKENBAUER


FIFA TEAM OF THE YEAR
1. Cassilas
2.Alves
3.Marcelo
4.Ramos
5.Pique
6.Alonso
7.C.Ronaldo
8.Iniesta
9.Falcao
10.Messi
11. Xavi




BALLON D'OR