Wednesday, January 23, 2013

Tangazo kwa wanafunzi wote wa BAPRM TWO-SAUT MWANZA

Jamani nimepewa vitabu na mwalimu Jota wa Enterpreneur ninavyo ktk flash amesema kila mtu asome,mara nyingi nipo chuo na nitavipeleka kwa dada Irene - Stationery tafadhali sana anayetaka anitafute 0712 553 980
by Dova Mcheshi- Mbunge PR TWO A

Monday, January 21, 2013

JE,HUU NI UBINADAMU???


Na;Dovakmwene John Mscheshi


Kifo ni kitu kinachoweza kumtokea mtu yoyote na wakati wowote kwani tunaamini ni mipango ya Mungu. Kifo hutokea katika mazingira tofauti ikiwa ni pamoja na maradhi, ajali mbalimbali, vita/mapigano, ugomvi na kadhalika.
Vifo vipo vya ghafla pasipo kutarajia, vingine vikitokana na kuugua muda mfupi au mrefu. Mtu anapofariki shughuli za mazishi huandaliwa ambapo waombolezaji hukusanyika nyumbani kwa marehemu au sehemu iliyopangwa na wanafamilia kwa msiba.
Pale kwenye maombolezo huwa na pilikapilika nyingi huku ratiba ya maandalizi ikitangazwa kila inapobidi. Waombolezaji huonekana katika makundi wakiteta huku wengine wakiwa wamejawa na simanzi.
Pamoja na ukweli huo, tabia hizi hazipendezi. Kwa mfano, lipo jambo moja au niseme tabia ambayo imezoeleka kwa waombolezaji wengi kuonekana wakijadili zaidi chanzo cha kifo cha marehemu badala ya kutafakari hatma yao waliobaki duniani na kumuombea aliyetangulia mbele za haki.
Kwa maneno mengine, wapo watu wanaogeuza msiba kama vijiwe vya kumjadili marehemu. Na watu hawa, hata wakati wa uhai wake hawakuwa kusema juu yake hadharani penye kadamnasi ya watu, lakini leo kafariki wanazusha hata yale yaliyofichika. Hebu tujiulize, hivi yanahusu? Na kwanini wanadamu tuko hivi? Hii ni kasoro kubwa sana yafaa tubadilike.
Utasikia fulani wakati wa uhai wake alikuwa anaringa sana. Ebo! Ulitaka afanyeje. Hivi hujui maringo ni afya na kinyume chake ni kasoro? Kuringa ni kujisikia furaha kwa uhai wako. Ndio, usibishe.
Mara utasikia fulani alikuwa kiruka njia, alipenda sana wanaume au wanawake, alipenda sana wake au waume za watu…Oh, ameacha watoto wa baba tofauti, amekufa na gonjwa baya, eti angezingatia ushauri wa daktari yasingemsibu hayo, ili mradi ni maneno ya hovyo, kisa anayezungumzwa ameshajifumzikia.
Wengine utasikia eti laana ya baba au mama yake ndio imemuua. Ili mradi mtu atoe neno kinywani mwake kufurahisha jopo pale kwenye maombolezo. Hili siyo jambo zuri hata kidogo, hasa ikizingatiwa kuwa kila mtu anayo mapungufu yake na hakuna atakayeishi milele nikiamini kile alichowahi kuniambia bibi yangu kuwa “Uyana nyi maseiyano” yaani “Dunia ni mapishano”.
Tabia nyingine inayokera wakati wa msiba ambayo wengi bado wanaiendekeza ni kule baadhi ya ndugu kugombea mali za marehemu zikiwemo nguo zake. Eti kufa kufaana na kwamba aliyekufa kafa hivyo mali zake ni halali kwa wengine. Lo! Makubwa kwani madogo yana unafuu.
Nimewahi kushuhudia ndugu wakichukua nguo za marehemu kwa kuzificha na kuondoka nazo, tena mwili wa marehemu ukiwa bado chumba cha maiti hospitalini. Yaani mwili haujazikwa, tayari watu wanajigawia mali zake. Ni tabia mbaya sana hii. Wenye tabia hii wasidhani ni kirahisi hivyo, yapo madhara yake. Kwanini mtu asisubiri kupewa mali chini ya taratibu za kifamilia?
Lingine ambalo halina sura nzuri walifanyalo wanadamu ni kule kukimbilia kuuona mwili wa marehemu wakati hapa alipokuwa mgonjwa hakuwahi kwenda kumjulia hali achilia mbali kumsaidia fedha za matibabu. Hukimbilia kuona kafa na afya yake au kakonda? Acheni jamani, mzaha huu, ni dhambi.
Mpenzi msomaji, hebu niulize; lipi ni jema katika haya mawili:- kumtembelea mgonjwa na ikibidi kumsaidia fedha za matibabu au kule kwenda mchanga rambirambi baada ya kufa?
Wapo wale ambao hawakujua fulani alikuwa mgonjwa, lakini wakasikia amefariki. Lakini wengine, pengine mahasimu waliowahi kukwaruzana, wakisia fulani kafa huachia; “acha afe”. Yaani hawaoni kwamba hiyo ni njia yao pia. Huu siyo ubinadamu. Maisha ya mtu yanapotoweka lazima usikitike kwani hutamuona tena katika maisha haya ya kidunia. Na utambue nawe kifo kinakusubiri.
Nakumbuka bibi mzaa mamangu wakati wa uhai wake kila nilipomtembelea alikuwa anafurahi sana pale ninapompelekea zawadi ambapo husema; “Afadhali uniletee watati ningali hai, kwani nikishafumba macho(kufa) utakachoniletea ni bure”. Yalikuwa ni maneno yaliyobeba ujumbe mzito sana.
Ndio maana ni muhimu sana hata pale mwenzako anapokuwa mgonjwa yafaa tumhudumie kwa nguvu zote, tumsaidie chakula, dawa badala ya kusubiri azimike ndipo tupige mikono mifukoni kutoa rambirambi.
Sisemi watu wasitoe rambirambi, la hasha. Ninachosema hapa ni kwamba tutizame mazingira yenyewe, kama ni kifo cha ghafla ni sawa. Lakini kama ni kifo kinachotokana na maradhi tusaidiane wakati wa uhai badala ya kubezana. Pengine msaada wako unaweza kumsogezea mgonjwa maisha akakamilisha mipango yake duniani au hata akapona kabisa. Maisha Ndivyo Yalivyo.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI     

Ajali yaua mmoja MBEYA.




Mtu mmoja amekufa papohapo na wengine 48 kujeruhiwa vibaya baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Jijini Mbeya kwenda Dar es Salaam kupinduka kwenye mteremko mkali wa Mlima Inyara nje kidogo ya Jiji la Mbeya.

Ajali hiyo mbaya ilitokea jana majira ya saa 1:30 asubuhi ikihusisha basi la kampuni ya Nganga Express lenye namba za usajili T 413 AVU lililoondoka Mbeya majira ya saa 1:00 kuelekea Dar es Salaam.

Akisimulia jinsi ajali hiyo ilivyotokea, dereva wa basi hilo, Alex Bunyinyiga alisema alipofika kwenye mteremko wa mlima Inyara, mahali ambapo pia kuna kona kali, aliona lori kubwa lililokuwa limeegeshwa upande wa kulia wa barabara.

Alisema alipolikaribia lori hilo, ghafla lilitokea gari lingine aina ya Fuso ambalo lilipita lori lililoegeshwa na kumfuata upande wake, hali ambayo ilisababisha watake kugongana uso kwa uso.

“Baada ya kuona tunaenda kugongana uso kwa uso, niliamua kukwepesha gari langu upande wa lori lililokuwa limeeegeshwa upande wa kulia kwangu na nikafanikiwa kulipita lori hilo kwa upande wake wa kulia, lakini nilipojaribu kurudisha gari langu likae barabarani liligoma na ndipo likapinduka,” alisema Bunyinyiga.

Shuhuda mwingine wa ajali hiyo, Noa Elias alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori aina ya fuso ambaye aliamua kulipita lori lililoharibika barabarani bila tahadhari na kutaka kugongana uso kwa uso na basi la Nganga.

Muuguzi wa Zamu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, Bilhuda Feruz amethibitisha kupokea majeruhi 48 na wanane kati yao wamelazwa na hali zao zinaendelea vizuri.

Hata hivyo, takwimu hizo zimetofautiana na zile zilizotolewa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athuman ambaye alidai kuwa majeruhi walikuwa ni 53 nwa kwamba 45 kati yao walitibiwa katika Hospitali ya Rufaa na kuruhusiwa huku majeruhi wanane wakilazwa hospitalini hapo kwa matibabu zaidi.

Kamanda Diwani alimtaja mtu aliyepoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Enock Lwila mkazi wa Mama John Jijini Mbeya.

Alisema marehemu huyo alikuwa na Sh. milioni 13 mfukoni ambazo ziliokolewa na askari waliowahi kwenye eneo la tukio.

Kamanda Diwani alisema kuwa kwa sasa fedha hizo ziko salama mikononi mwa Polisi na kuwa baada ya kupatikana kwa ndugu halali wa marehemu atakabidhiwa.

 
CHANZO: NIPASHE     

RC Lindi alazwa,Pinda amtembelea


Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovick Mwananzila, amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

Akizungumza na NIPASHE jana mmoja wa wanafamilia ambaye alipokea simu ya Mkuu huyo wa mkoa alisema Mwananzila amelazwa hospitalini hapo tangu Jumatano ya wiki iliyopita.
Alisema Waziri Mkuu Mizengo Pinda amemtembela jana kumjulia hali na kwamba hata hivyo anaendelea vizuri na madaktari wamekuwa karibu naye kumtibu.

Naye Ofisa habari wa Muhimbili, Aminael Aligaesha, alisema Mkuu wa Mkoa wa Lindi hali yake inaendelea vizuri ukilinganisha na siku alipopelekwa hospitalini hapo.

OKAH matatani huko Afrika kusini








Mahakama nchini Afrika Kusini imempata na hatia ya vitendo vya kigaidi kiongozi wa waasi wa Nigeria Henry Okah.

Okah anasemekana kupanga mashambulizi ya mabomu yaliyotegwa ndani ya gari na kuwaua watu 12.
Taarifa zinazohusiana
Afrika

Okah alipatikana na hatia ya makosa 13 kuhusiana na vitendo vya kigaidi.

Alikamatwa mjini Johannesburg siku moja baada ya mabomu mawili kulipuka wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Nigeria.

Alikanusha makosa hayo ingawa kundi analoongoza la Mend, lilikiri kutekeleza mashambulizi hayo.

Jaji wa mahakama kuu mjini Johannesburg, Neels Claassen, alimpata na hatia Okah ya makosa ya kupanga njama ya mashambulizi pamoja na kufanya vitendo vya kigaidi ikiwemo kulipua mabomu.

"ushahidi ambao ulitolewa na washirika wake haukupingana,'' alisema jaji Claassen

Okah alikamatwa kwa kosa la kumiliki bunduki kinyume na sheria nchini Angola mwaka 2007 na kisha kuhamishwa hadi nchini Nigeria ingawa hakuwahi kuhukumiwa.

Aliachiliwa baada ya miaka miwili chini ya msamaha uliotolewa kwa wapiganaji walio katika maeneo ya mafuta na ndipo aliporejea Afrika Kusini ambako aliishi hadi mwaka 2003.

MAN UNITED YABANWA.


Robin Van Persie aliiwezesha timu yake ya Manchester United kuongoza kipindi cha kwanza baada ya kufunga bao katika dakika ya 25.
Taarifa zinazohusiana
Kandanda, Uingereza

Van Persie alipata goli hilo akiunganisha krosi ya Tom Cleverly.

Man United wakiamini kuwa tayari wamepata ushindi katika mechi hiyo, walijikuta wakigawa pointi baada ya Clint Dempsey kufunga katika dakika za majeruhi na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa Tottenham katika uwanja wao wa White Hart Lane.

Matokeo hayo bado yanaiacha Manchester United kileleni mwa ligi hiyo ikiwa na pointi 56, huku ikifuatiwa na Manchester City yenye pointi 51.

Tottenham iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 41, pointi nne nyuma ya Chelsea yenye pointi 45, ikikakalia nafasi ya tatu ya ligi kuu ya England.

Timu zote hizo nne zimecheza mechi 23 kila moja.




MALI YAVUNA POINTI 3 MUHIMU-AFCON




Seydou Keita Keita baada ya kufunga bao lake la kwanza dhidi ya Niger


Mali inayopewa nafasi ya kusonga katika hatua ya makundi, ya michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika, mwaka huu, imeandikisha ushindi wake wa kwanza katika mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Niger.

Mali iliilaza Niger bao moja kwa bila katika mechi hiyo ya pili ya kundi B.

Seydou Keita, nahodha wa timu ya Mali, alifunga bao hilo la ushindi katika dakika ya 84 baada ya mlinda mlango wa Niger, Daouda Kassaly, kuutema mpira wa adhabu na kumfikia mfungaji.

Kwa matokeo hayo Mali, sasa inaongoza kundi B ikiwa na pointi tatu na goli moja.

Timu za DRC na Ghana zinafuatia katika msimamo wa kundi B, zikiwa na pointi moja kila moja baada ya timu hizo mbili kutoshana nguvu ya kufunga magoli mawili kwa mawili.

Hapo kesho mechi za kundi C, zinaanza huku mabingwa watetezi Zambia wakimenyana na Ethiopia, nayo Nigeria ikivaana na Burkina Faso.