Monday, January 21, 2013

OKAH matatani huko Afrika kusini








Mahakama nchini Afrika Kusini imempata na hatia ya vitendo vya kigaidi kiongozi wa waasi wa Nigeria Henry Okah.

Okah anasemekana kupanga mashambulizi ya mabomu yaliyotegwa ndani ya gari na kuwaua watu 12.
Taarifa zinazohusiana
Afrika

Okah alipatikana na hatia ya makosa 13 kuhusiana na vitendo vya kigaidi.

Alikamatwa mjini Johannesburg siku moja baada ya mabomu mawili kulipuka wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Nigeria.

Alikanusha makosa hayo ingawa kundi analoongoza la Mend, lilikiri kutekeleza mashambulizi hayo.

Jaji wa mahakama kuu mjini Johannesburg, Neels Claassen, alimpata na hatia Okah ya makosa ya kupanga njama ya mashambulizi pamoja na kufanya vitendo vya kigaidi ikiwemo kulipua mabomu.

"ushahidi ambao ulitolewa na washirika wake haukupingana,'' alisema jaji Claassen

Okah alikamatwa kwa kosa la kumiliki bunduki kinyume na sheria nchini Angola mwaka 2007 na kisha kuhamishwa hadi nchini Nigeria ingawa hakuwahi kuhukumiwa.

Aliachiliwa baada ya miaka miwili chini ya msamaha uliotolewa kwa wapiganaji walio katika maeneo ya mafuta na ndipo aliporejea Afrika Kusini ambako aliishi hadi mwaka 2003.

No comments:

Post a Comment